Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira Nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake huwaka upesi; Heri wote wanaomkimbilia.
Mathayo 28:17 - Swahili Revised Union Version Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao walikuwa na mashaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walipomwona wakamwabudu, ingawa wengine walikuwa na mashaka. Biblia Habari Njema - BHND Walipomwona wakamwabudu, ingawa wengine walikuwa na mashaka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walipomwona wakamwabudu, ingawa wengine walikuwa na mashaka. Neno: Bibilia Takatifu Walipomwona, wakamwabudu; lakini baadhi yao wakaona shaka. Neno: Maandiko Matakatifu Walipomwona, wakamwabudu; lakini baadhi yao wakaona shaka. BIBLIA KISWAHILI Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao walikuwa na mashaka. |
Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira Nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake huwaka upesi; Heri wote wanaomkimbilia.
Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.
Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia.
Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutoamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu.
ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyemtuma.
wale aliojidhihirisha kwao kuwa yu hai, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, akiwatokea muda wa siku arubaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.
baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala;