Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa ushauri wake haukufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajinyonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.
Mathayo 27:5 - Swahili Revised Union Version Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naye akazitupa zile fedha hekaluni, akatoka nje, akaenda akajinyonga. Biblia Habari Njema - BHND Naye akazitupa zile fedha hekaluni, akatoka nje, akaenda akajinyonga. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naye akazitupa zile fedha hekaluni, akatoka nje, akaenda akajinyonga. Neno: Bibilia Takatifu Basi Yuda akavitupa vile vipande vya fedha ndani ya Hekalu akaondoka akaenda kujinyonga. Neno: Maandiko Matakatifu Basi Yuda akavitupa vile vipande vya fedha ndani ya Hekalu akaondoka akaenda kujinyonga. BIBLIA KISWAHILI Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga. |
Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa ushauri wake haukufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajinyonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.
Ikawa Zimri alipoona ya kuwa mji umetwaliwa, akaingia ngomeni mwa nyumba ya mfalme, akaiteketeza nyumba ya mfalme juu yake kwa moto, akafa;
Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Mkufuru Mungu, ufe.
Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Na baadaye wawili wakatokea, wakasema, Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu la Mungu, na kulijenga kwa siku tatu.
Wakuu wa makuhani wakavitwaa vile vipande vya fedha, wakasema, Si halali kuviweka katika sanduku ya sadaka, kwa kuwa ni fedha ya damu.
kama ilivyokuwa desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba.
Ndipo akamwita kwa haraka huyo kijana aliyekuwa anamchukulia silaha zake, na kumwambia, Futa upanga wako, uniue, ili watu wasiseme juu yangu, Aliuawa na mwanamke. Basi huyo kijana wake akamchoma upanga, naye akafa.