Mathayo 26:43 - Swahili Revised Union Version Akaja tena, akawakuta wamelala; maana macho yao yalijawa na usingizi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi. Biblia Habari Njema - BHND Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akawaendea tena, akawakuta wamelala, maana macho yao yalikuwa yamebanwa na usingizi. Neno: Bibilia Takatifu Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. Neno: Maandiko Matakatifu Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. BIBLIA KISWAHILI Akaja tena, akawakuta wamelala; maana macho yao yalijawa na usingizi. |
Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee.
Akaenda tena mara ya pili, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniondokee nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe.
Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi; lakini walipokwisha amka waliuona utukufu wake, na wale wawili waliosimama pamoja naye.
Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka ghorofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa.
Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.