Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali hasira yake itakuwa juu yake aletaye aibu.
Mathayo 24:47 - Swahili Revised Union Version Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kweli nawaambieni, atamweka mtumishi huyo aisimamie mali yake yote. Biblia Habari Njema - BHND Kweli nawaambieni, atamweka mtumishi huyo aisimamie mali yake yote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kweli nawaambieni, atamweka mtumishi huyo aisimamie mali yake yote. Neno: Bibilia Takatifu Amin, nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. Neno: Maandiko Matakatifu Amin, nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. BIBLIA KISWAHILI Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. |
Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali hasira yake itakuwa juu yake aletaye aibu.
Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.
Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.
Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi;
Yeye ashindaye, nitamridhia kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.