Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
Mathayo 24:26 - Swahili Revised Union Version Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, wakiwaambieni, ‘Tazameni, yuko jangwani,’ msiende huko; au, ‘Tazameni, amejificha ndani,’ msisadiki; Biblia Habari Njema - BHND Basi, wakiwaambieni, ‘Tazameni, yuko jangwani,’ msiende huko; au, ‘Tazameni, amejificha ndani,’ msisadiki; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, wakiwaambieni, ‘Tazameni, yuko jangwani,’ msiende huko; au, ‘Tazameni, amejificha ndani,’ msisadiki; Neno: Bibilia Takatifu “Basi mtu yeyote akiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msiende huko. Au akisema, ‘Yuko kwenye chumba,’ msisadiki. Neno: Maandiko Matakatifu “Kwa hiyo mtu yeyote akiwaambia, ‘Yule kule nyikani,’ msiende huko. Au akisema, ‘Yuko kwenye chumba,’ msisadiki. BIBLIA KISWAHILI Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. |
Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
Wewe si yule Mmisri ambaye kabla ya siku hizi aliwafitinisha wale watu elfu nne, walioitwa Wauaji, akawaongoza jangwani?