Mathayo 23:11 - Swahili Revised Union Version Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu. Biblia Habari Njema - BHND Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu. Neno: Bibilia Takatifu Yeye aliye mkuu kuliko ninyi nyote miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye aliye mkuu kuliko ninyi nyote miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu. BIBLIA KISWAHILI Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. |
Akaketi chini, akawaita wale Kumi na Wawili akawaambia, Mtu atakaye kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote, na mtumishi wa wote.
Maana, ingawa nimekuwa huru kwa watu wote, nilijifanya mtumwa wa wote, ili nipate watu wengi zaidi.
Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi.
Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.
Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.