Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
Mathayo 21:22 - Swahili Revised Union Version Na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Na mkiwa na imani, chochote mtakachoomba kwa sala, mtapata.” Biblia Habari Njema - BHND Na mkiwa na imani, chochote mtakachoomba kwa sala, mtapata.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Na mkiwa na imani, chochote mtakachoomba kwa sala, mtapata.” Neno: Bibilia Takatifu Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea.” Neno: Maandiko Matakatifu Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea.” BIBLIA KISWAHILI Na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. |
Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu zawadi njema, je! Si Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema zaidi wao wamwombao?
Kwa sababu hiyo nawaambia, Yoyote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa.
Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.
Basi ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Sala yake mwenye haki ina nguvu nyingi, na hutenda mengi.
na lolote tuombalo, tunalipokea kwake, kwa kuwa tunazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.