na hao nao akawaambia, Nendeni nanyi pia katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.
Mathayo 20:5 - Swahili Revised Union Version Akatoka tena mnamo saa sita na saa tisa, akafanya vile vile. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, wakaenda. Huyo mwenye shamba akatoka tena mnamo saa sita na saa tisa, akafanya vivyo hivyo. Biblia Habari Njema - BHND Basi, wakaenda. Huyo mwenye shamba akatoka tena mnamo saa sita na saa tisa, akafanya vivyo hivyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, wakaenda. Huyo mwenye shamba akatoka tena mnamo saa sita na saa tisa, akafanya vivyo hivyo. Neno: Bibilia Takatifu Hivyo basi wakaenda. “Akatoka tena mnamo saa sita na pia saa tisa akafanya vivyo hivyo. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo wakaenda. “Akatoka tena mnamo saa sita na pia saa tisa akafanya vivyo hivyo. BIBLIA KISWAHILI Akatoka tena mnamo saa sita na saa tisa, akafanya vile vile. |
na hao nao akawaambia, Nendeni nanyi pia katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda.
Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
Akawaambia, Njooni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.
Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.
Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.
Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio!
Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana;