Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari.
Mathayo 20:11 - Swahili Revised Union Version Basi wakiisha kuipokea, wakamnung'unikia mwenye nyumba, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakazipokea fedha zao, wakaanza kumnungunikia yule bwana. Biblia Habari Njema - BHND Wakazipokea fedha zao, wakaanza kumnungunikia yule bwana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakazipokea fedha zao, wakaanza kumnung'unikia yule bwana. Neno: Bibilia Takatifu Walipoipokea, wakaanza kulalamika dhidi ya yule mwenye shamba, Neno: Maandiko Matakatifu Walipoipokea, wakaanza kulalamika dhidi ya yule mwenye shamba, BIBLIA KISWAHILI Basi wakiisha kuipokea, wakamnung'unikia mwenye nyumba, |
Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari.
wakisema, Hao wa mwisho wamefanya kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na joto la mchana kutwa.
Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung'unikia sana yule mwanamke.
Mafarisayo na waandishi wakanung'unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao.
Hata watu walipoona, walinung'unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi.
Ikawa Mafarisayo na waandishi wao kuwanung'unikia wanafunzi wake, wakisema, Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?
Basi Wayahudi wakamnung'unikia, kwa sababu alisema, Mimi ni chakula kilichoshuka kutoka mbinguni.
Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung'unikia neno hilo, akawaambia, Je! Neno hili linawakwaza?
Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana.
huku wakituzuia tusiseme na Mataifa wapate kuokolewa; ili watimize dhambi zao siku zote. Lakini hasira imewafikia hata mwisho.
Watu hawa ni wenye kunung'unika, wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao, na vinywa vyao vyanena maneno makuu mno ya kiburi, wakipendelea watu wenye cheo kwa ajili ya faida.