Mikaya akasema, Ukirudi kabisa kwa amani, BWANA hakusema kwa mimi. Akasema, Sikieni, enyi watu wote.
Mathayo 15:10 - Swahili Revised Union Version Akawaita makutano akawaambia Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu aliuita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni, mkaelewe! Biblia Habari Njema - BHND Yesu aliuita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni, mkaelewe! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu aliuita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni, mkaelewe! Neno: Bibilia Takatifu Isa akaita umati wa watu waliokuwa hapo, akawaambia, “Sikilizeni na mwelewe: Neno: Maandiko Matakatifu Isa akaita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni na mwelewe: BIBLIA KISWAHILI Akawaita makutano akawaambia |
Mikaya akasema, Ukirudi kabisa kwa amani, BWANA hakusema kwa mimi. Akasema, Sikieni, enyi watu wote.
Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.
Naye akaniambia, Nenda, ukawaambie watu hawa, Endeleeni kusikia, lakini msifahamu; endeleeni kutazama, lakini msione.
Kila mtu alisikiapo neno la ufalme bila kulielewa, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.
Sikilizeni, mfahamu; Sicho kiingiacho kinywani kimtiacho mtu unajisi; bali kitokacho kinywani ndicho kimtiacho mtu unajisi.
Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;
Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;
Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.