Mathayo 14:25 - Swahili Revised Union Version Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usiku, karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji. Biblia Habari Njema - BHND Usiku, karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usiku, karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji. Neno: Bibilia Takatifu Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Isa akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Isa akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. BIBLIA KISWAHILI Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari. |
Na kuziweka nguzo za ghorofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, Na kwenda juu ya mabawa ya upepo,
Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliujua ule wakati mwizi atakaokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.
Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jogoo, au asubuhi;
Akawaona wakitaabika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa unwakabili; hata ilipopata kama zamu ya nne ya usiku akawaendea, akitembea juu ya bahari; akataka kuwapita.
Basi wakavuta makasia kadiri ya maili tatu nne, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari na kuikaribia mashua; wakaogopa.
Na katika mkono wake alikuwa na kitabu kidogo kimefunguliwa. Akaweka mguu wake wa kulia juu ya bahari, nao wa kushoto juu ya nchi.
Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kulia kuelekea mbinguni,
Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Nenda, ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mkono wa yule malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi.