Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.
Mathayo 13:51 - Swahili Revised Union Version Yesu aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akawauliza, “Je, mmeelewa mambo haya yote?” Wakamjibu, “Naam.” Biblia Habari Njema - BHND Yesu akawauliza, “Je, mmeelewa mambo haya yote?” Wakamjibu, “Naam.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akawauliza, “Je, mmeelewa mambo haya yote?” Wakamjibu, “Naam.” Neno: Bibilia Takatifu Isa akauliza, “Je, mmeyaelewa haya yote?” Wakamjibu, “Ndiyo.” Neno: Maandiko Matakatifu Isa akauliza, “Je, mmeyaelewa haya yote?” Wakamjibu, “Ndiyo.” BIBLIA KISWAHILI Yesu aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam. |
Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.
Kila mtu alisikiapo neno la ufalme bila kulielewa, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.
Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.
Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa sikuwaambia kwa sababu ya mkate? Ila jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.
Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu),
wala pasipo mfano hakusema nao; lakini akawaeleza wanafunzi wake mwenyewe mambo yote kwa faragha.
Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;
Nasi tunajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.