Mathayo 12:3 - Swahili Revised Union Version Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma alivyofanya Daudi pamoja na wenzake wakati walipokuwa na njaa? Biblia Habari Njema - BHND Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma alivyofanya Daudi pamoja na wenzake wakati walipokuwa na njaa? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akawajibu, “Je, hamjasoma alivyofanya Daudi pamoja na wenzake wakati walipokuwa na njaa? Neno: Bibilia Takatifu Isa akawajibu, “Je, hamjasoma alichofanya Daudi na wenzake walipokuwa na njaa? Neno: Maandiko Matakatifu Isa akawajibu, “Je, hamjasoma alichofanya Daudi na wenzake walipokuwa na njaa? BIBLIA KISWAHILI Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe? |
Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.
Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao?
Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato pasipo kupata hatia?
Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mwanamume na mwanamke,
wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umejiandalia sifa?
Hata andiko hili hamjalisoma, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Na kuhusu wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, Kuhusu kile kichaka jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?
Yesu akawajibu akawaambia, Hamkulisoma hata hilo alilolifanya Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wale aliokuwa nao?