Siku sita utafanya kazi yako, na siku ya saba utapumzika; ili kwamba ng'ombe wako na punda wako wapate kupumzika, kisha mwana wa mjakazi wako na mgeni wapate kuburudika.
Mathayo 12:2 - Swahili Revised Union Version Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo ambalo si halali kulifanya siku ya sabato. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, “Tazama, wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanya siku ya Sabato.” Biblia Habari Njema - BHND Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, “Tazama, wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanya siku ya Sabato.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, “Tazama, wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanya siku ya Sabato.” Neno: Bibilia Takatifu Lakini Mafarisayo walipoona jambo hili, wakamwambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato.” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Mafarisayo walipoona jambo hili, wakamwambia, “Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo lisilo halali kufanywa siku ya Sabato.” BIBLIA KISWAHILI Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama! Wanafunzi wako wanafanya jambo ambalo si halali kulifanya siku ya sabato. |
Siku sita utafanya kazi yako, na siku ya saba utapumzika; ili kwamba ng'ombe wako na punda wako wapate kupumzika, kisha mwana wa mjakazi wako na mgeni wapate kuburudika.
Fanyeni kazi siku sita, lakini siku ya saba itakuwa siku takatifu kwenu; ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa BWANA; mtu yeyote atakayefanya kazi yoyote katika siku hiyo atauawa.
Kama ukigeuza mguu wako usiivunje sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe;
Na tazama, yumo mtu mwenye mkono umepooza; wakamwuliza, wakisema, Ni halali kuponya watu siku ya sabato? Ili wapate kumshitaki.
Yesu akajibu, akawaambia wanasheria na Mafarisayo, Je! Ni halali kuponya siku ya sabato, ama sivyo?
Wakarudi, wakatayarisha manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa.