Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.
Mathayo 11:13 - Swahili Revised Union Version Kwa maana manabii wote na Torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mafundisho yote ya manabii na sheria mpaka wakati wa Yohane yalibashiri juu ya nyakati hizi. Biblia Habari Njema - BHND Mafundisho yote ya manabii na sheria mpaka wakati wa Yohane yalibashiri juu ya nyakati hizi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mafundisho yote ya manabii na sheria mpaka wakati wa Yohane yalibashiri juu ya nyakati hizi. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana manabii wote na Torati walitabiri hadi wakati wa Yahya. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana manabii wote na Torati walitabiri mpaka wakati wa Yahya. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana manabii wote na Torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. |
Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.
Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu huuteka.
Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa ningali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika vitabu vya Manabii na Zaburi.
Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu.
Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na Torati na Manabii;