Lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.
Matendo 8:4 - Swahili Revised Union Version Lakini wale waliotawanyika wakaenda huku na huko wakilihubiri neno. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wale waumini waliotawanyika, walikwenda kila mahali wakihubiri ule ujumbe. Biblia Habari Njema - BHND Wale waumini waliotawanyika, walikwenda kila mahali wakihubiri ule ujumbe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wale waumini waliotawanyika, walikwenda kila mahali wakihubiri ule ujumbe. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo wale waliotawanyika wakalihubiri neno la Mungu kila mahali walipoenda. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo wale waliotawanyika wakalihubiri neno la Mungu kila mahali walipokwenda. BIBLIA KISWAHILI Lakini wale waliotawanyika wakaenda huku na huko wakilihubiri neno. |
Lakini watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawaambia, Hamtaimaliza miji ya Israeli, hata ajapo Mwana wa Adamu.
kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neno tokea mwanzo,
Basi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile dhiki iliyotukia kwa habari ya Stefano, wakasafiri hadi Foinike na Kipro na Antiokia, wasilihubiri lile neno ila kwa Wayahudi peke yao.
Na Paulo na Barnaba wakakaa huko Antiokia, wakifundisha na kulihubiri neno la Bwana, pamoja na watu wengine wengi.
Siku ile kukatokea mateso makuu kwa kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Yudea na Samaria, isipokuwa hao mitume.
Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri Habari Njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
ingawa tuliteswa na kutukanwa, katika Filipi kama mjuavyo, tulithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.