Matendo 15:6 - Swahili Revised Union Version Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulitafakari neno hilo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, mitume na wazee walifanya mkutano maalumu wa kuchunguza jambo hilo. Biblia Habari Njema - BHND Basi, mitume na wazee walifanya mkutano maalumu wa kuchunguza jambo hilo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, mitume na wazee walifanya mkutano maalumu wa kuchunguza jambo hilo. Neno: Bibilia Takatifu Mitume na wazee wakakutana pamoja ili kufikiri jambo hili. Neno: Maandiko Matakatifu Mitume na wazee wakakutana pamoja ili kufikiri jambo hili. BIBLIA KISWAHILI Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulitafakari neno hilo. |
Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee ili kuzungumza juu ya suala hilo.
Basi ikawapendeza mitume na wazee na kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba; nao ni hawa, Yuda aliyeitwa Barsaba, na Sila, waliokuwa watu wakuu katika ndugu. Wakaandika hivi na kupeleka kwa mikono yao,
sisi tumeona vema, hali tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwatuma kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo,
Walipofika Yerusalemu wakakaribishwa na kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.
Basi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemu, ili wazishike.
Wale Kumi na Wawili wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani.
Watiini viongozi wenu, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa huzuni; maana haitawafaa ninyi.
Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.