Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Matendo 13:18 - Swahili Revised Union Version

Na kwa muda wa miaka kama arubaini akawavumilia katika jangwa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Aliwavumilia kwa muda wa miaka arubaini kule jangwani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Aliwavumilia kwa muda wa miaka arubaini kule jangwani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Aliwavumilia kwa muda wa miaka arubaini kule jangwani.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa muda wa miaka arobaini alivumilia matendo yao walipokuwa jangwani.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa muda wa miaka arobaini alivumilia matendo yao walipokuwa jangwani.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na kwa muda wa miaka kama arobaini akawavumilia katika jangwa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Matendo 13:18
19 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini miaka mingi ukachukuliana nao, nawe ukawashuhudia kwa roho yako kwa vinywa vya manabii wako; wao wasitake kusikiliza; kwa hiyo ukawatia katika mikono ya watu wa nchi.


Na mkutano mzima wa wana wa Israeli ukawanung'unikia Musa na Haruni, huko barani;


Na wana wa Israeli walikula Mana muda wa miaka arubaini, hata walipofikia nchi iliyo na watu, wakala ile Mana, hata walipofikia mipakani mwa nchi ya Kanaani.


kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu;


Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika Bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arubaini.


na huko jangwani, ulipoona alivyokuchukua BWANA, Mungu wako, kama mtu amchukuavyo mwanawe, njia yote mliyoiendea, hata mkafika mahali hapa.


Kumbuka, usisahau ulivyomtia BWANA, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hadi mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya BWANA