Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Marko 9:23 - Swahili Revised Union Version

Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Yesu akamwambia, “Ati ikiwa waweza! Mambo yote yanawezekana kwa mtu aliye na imani.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Yesu akamwambia, “Ati ikiwa waweza! Mambo yote yanawezekana kwa mtu aliye na imani.”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Yesu akamwambia, “Ati ikiwa waweza! Mambo yote yanawezekana kwa mtu aliye na imani.”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Isa akamwambia, “Ati, ‘Kama unaweza kufanya jambo lolote’? Yote yawezekana kwake yeye aaminiye.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Isa akamwambia, “Kama ukiweza kuamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Marko 9:23
12 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.


Akasema, Njoo. Petro akashuka katika mashua, akatembea juu ya maji, ili kumwendea Yesu.


Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu. [


Amin, nawaambia, yeyote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.


Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lolote, utuhurumie, na kutusaidia.


Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutoamini kwangu.


Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.


Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?


Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; naye Paulo akamkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa,


Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.