Marko 9:21 - Swahili Revised Union Version Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Amepatwa na mambo hayo tangu lini?” Naye akamjibu, “Tangu utoto wake. Biblia Habari Njema - BHND “Amepatwa na mambo hayo tangu lini?” Naye akamjibu, “Tangu utoto wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Amepatwa na mambo hayo tangu lini?” Naye akamjibu, “Tangu utoto wake. Neno: Bibilia Takatifu Isa akamuuliza baba yake, “Mwanao amekuwa katika hali hii tangu lini?” Akamjibu, “Tangu utoto wake. Neno: Maandiko Matakatifu Isa akamuuliza baba yake, “Mwanao amekuwa katika hali hii tangu lini?” Akamjibu, “Tangu utoto wake. BIBLIA KISWAHILI Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, Tangu utoto. |
Wakamleta kwake; hata alipomwona, mara yule pepo alimtia kifafa; naye akaanguka chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu.
Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lolote, utuhurumie, na kutusaidia.
Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Abrahamu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato?
Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu yeyote,
Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja, asiyeweza kutumia miguu yake na aliyekuwa kiwete tangu kuzaliwa kwake.
Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu.
Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, mtu huyo alikuwa amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza.