Marko 8:21 - Swahili Revised Union Version Akawaambia, Hamjafahamu bado? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, akawaambia, “Na bado hamjaelewa?” Biblia Habari Njema - BHND Basi, akawaambia, “Na bado hamjaelewa?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, akawaambia, “Na bado hamjaelewa?” Neno: Bibilia Takatifu Ndipo akawauliza, “Je, bado hamwelewi?” Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo akawauliza, “Je, bado hamwelewi?” BIBLIA KISWAHILI Akawaambia, Hamjafahamu bado? |
Akapiga kite rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki.
Naye Yesu akatambua, akawaambia, Mbona mnabishana kwa sababu hamna mikate? Hamfahamu bado, wala hamjaelewa? Je! Mioyo yenu ni mizito?
Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hadi lini? Nichukuliane nanyi hadi lini? Mleteni kwangu.
Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuoneshe Baba?
Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.
Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake?