Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.
Marko 7:14 - Swahili Revised Union Version Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu aliuita tena ule umati wa watu, akawaambia, “Nisikilizeni nyote, mkaelewe. Biblia Habari Njema - BHND Yesu aliuita tena ule umati wa watu, akawaambia, “Nisikilizeni nyote, mkaelewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu aliuita tena ule umati wa watu, akawaambia, “Nisikilizeni nyote, mkaelewe. Neno: Bibilia Takatifu Isa akaita tena umati ule wa watu, akawaambia, “Nisikilizeni nyote, na mwelewe jambo hili. Neno: Maandiko Matakatifu Isa akaita tena ule umati wa watu, akawaambia, “Nisikilizeni, kila mmoja wenu na mwelewe jambo hili. BIBLIA KISWAHILI Akawaita makutano tena, akawaambia, Nisikieni nyote na kufahamu. |
Naye Eliya akawakaribia watu wote, akanena, Mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye. Wale watu hawakumjibu neno.
Mikaya akasema, Ukirudi kabisa kwa amani, BWANA hakusema kwa mimi. Akasema, Sikieni, enyi watu wote.
Naye akaniambia, Nenda, ukawaambie watu hawa, Endeleeni kusikia, lakini msifahamu; endeleeni kutazama, lakini msione.
ambalo Yeremia, nabii, aliwaambia watu wote wa Yuda, na wenyeji wote wa Yerusalemu, kusema,
huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokezana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.
Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu. [
Wakati huo, makutano walipokutanika maelfu, hata wakakanyagana, alianza kuwaambia wanafunzi wake kwanza, Jilindeni na chachu ya Mafarisayo, ambayo ni unafiki.
Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma kitabu cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma?