Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.
Marko 6:46 - Swahili Revised Union Version Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya kuwaaga watu alikwenda mlimani kusali. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya kuwaaga watu alikwenda mlimani kusali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya kuwaaga watu alikwenda mlimani kusali. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya kuwaaga, akaenda mlimani kuomba. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kuomba. BIBLIA KISWAHILI Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba. |
Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.
Na kulipokuwa jioni mashua ilikuwa katikati ya bahari, na yeye yu peke yake katika nchi kavu.
Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.
Baada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi, kisha akaagana na ndugu akaabiri kwenda Shamu; na Priskila na Akila wakaenda pamoja naye, alipokwisha kunyoa kichwa chake huko Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri.
bali aliagana nao, akisema, Nitarejea kwenu tena, Mungu akinijalia. Akatweka, akatoka Efeso,
sikuona raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia.
Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.