Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa kuwa anaendelea kutupigia makelele nyuma yetu.
Marko 6:36 - Swahili Revised Union Version uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Afadhali uwaage watu waende mashambani na katika vijiji vya jirani, wanunue chakula.” Biblia Habari Njema - BHND Afadhali uwaage watu waende mashambani na katika vijiji vya jirani, wanunue chakula.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Afadhali uwaage watu waende mashambani na katika vijiji vya jirani, wanunue chakula.” Neno: Bibilia Takatifu Waage watu ili waende mashambani na vijijini jirani, wakajinunulie chakula.” Neno: Maandiko Matakatifu Waage watu ili waende mashambani na vijijini jirani, wakajinunulie chakula.” BIBLIA KISWAHILI uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula. |
Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa kuwa anaendelea kutupigia makelele nyuma yetu.
Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.
Wanafunzi wake wakamwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusongasonga, nawe wasema, Ni nani aliyenigusa?
Hata zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa;
Akajibu, akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakamwambia, Je! Twende tukanunue mikate ya dinari mia mbili ili tuwape kula?