Marko 4:4 - Swahili Revised Union Version ikawa alipokuwa akipanda, mbegu nyingine ilianguka kando ya njia, wakaja ndege wakaila. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila. Biblia Habari Njema - BHND Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila. Neno: Bibilia Takatifu Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila. Neno: Maandiko Matakatifu Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila. BIBLIA KISWAHILI ikawa alipokuwa akipanda, mbegu nyingine ilianguka kando ya njia, wakaja ndege wakaila. |
Kila mtu alisikiapo neno la ufalme bila kulielewa, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.
Hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, mara huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao.
Nyingine ikaanguka penye mwamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara ikaota kwa kuwa na udongo haba;
Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka.
Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila.