Marko 4:36 - Swahili Revised Union Version Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyokuwa katika mashua. Na mashua zingine zilikuwako pamoja naye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, wakauacha ule umati wa watu, wakamchukua Yesu katika mashua alimokuwa. Vilevile mashua nyingine zilimfuata. Biblia Habari Njema - BHND Basi, wakauacha ule umati wa watu, wakamchukua Yesu katika mashua alimokuwa. Vilevile mashua nyingine zilimfuata. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, wakauacha ule umati wa watu, wakamchukua Yesu katika mashua alimokuwa. Vilevile mashua nyingine zilimfuata. Neno: Bibilia Takatifu Wakaacha umati wa watu, na wakamchukua vile alivyokuwa kwenye mashua. Palikuwa pia na mashua zingine nyingi pamoja naye. Neno: Maandiko Matakatifu Wakauacha ule umati wa watu, na wakamchukua vile alivyokuwa kwenye mashua. Palikuwa pia na mashua nyingine nyingi pamoja naye. BIBLIA KISWAHILI Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyokuwa katika mashua. Na mashua zingine zilikuwako pamoja naye. |
Akawaambia wanafunzi wake ya kwamba mashua ndogo ikae karibu naye, kwa sababu ya mkutano, wasije wakamsonga.
Akaanza kufundisha tena kando ya ziwa. Kundi kubwa sana la watu wakamkusanyikia, hata yeye akapanda katika mashua, akakaa ziwani, watu wote walikuwa katika nchi kavu kando ya ziwa.
Na alipokwisha kushuka katika mashua, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu;
Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng'ambo katika ile mashua, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.
Ikawa siku zile mojawapo alipanda katika mashua yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa. Wakatweka matanga.