Nikushuhudie nini? Nikufananishe na nini, Ee Binti Yerusalemu? Nikulinganishe na nini, nipate kukufariji, Ee bikira binti Sayuni? Kwa maana uvunjifu wako ni mkuu kama bahari, Ni nani awezaye kukuponya?
Marko 4:30 - Swahili Revised Union Version Akasema, Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? Au tuutie katika mfano gani? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tena, Yesu akasema, “Tuufananishe Ufalme wa Mungu na nini? Tuueleze kwa mifano gani? Biblia Habari Njema - BHND Tena, Yesu akasema, “Tuufananishe Ufalme wa Mungu na nini? Tuueleze kwa mifano gani? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tena, Yesu akasema, “Tuufananishe Ufalme wa Mungu na nini? Tuueleze kwa mifano gani? Neno: Bibilia Takatifu Akawaambia tena, “Tuufananishe ufalme wa Mungu na nini? Au tutumie mfano gani ili kuueleza? Neno: Maandiko Matakatifu Akawaambia tena, “Tuufananishe Ufalme wa Mwenyezi Mungu na nini? Au tutumie mfano gani ili kuueleza? BIBLIA KISWAHILI Akasema, Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? Au tuutie katika mfano gani? |
Nikushuhudie nini? Nikufananishe na nini, Ee Binti Yerusalemu? Nikulinganishe na nini, nipate kukufariji, Ee bikira binti Sayuni? Kwa maana uvunjifu wako ni mkuu kama bahari, Ni nani awezaye kukuponya?
Lakini nitakifananisha na nini kizazi hiki? Kimefanana na watoto wanaokaa sokoni, wanaowaita wenzao, wakisema,
Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika shamba lake;
Ni kama punje ya haradali, ambayo ipandwapo katika nchi, ingawa ni ndogo kuliko mbegu zote zilizo katika nchi,