Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
Marko 4:22 - Swahili Revised Union Version Kwa maana hakuna neno lililositirika, ila kusudi lije kudhihirika; wala hakuna lililofichwa, ila kusudi lije kutokea wazi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila kilichofunikwa kitafunuliwa. Biblia Habari Njema - BHND Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila kilichofunikwa kitafunuliwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila kilichofunikwa kitafunuliwa. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna jambo lolote la siri ambalo halitaletwa nuruni. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna jambo lolote la siri ambalo halitaletwa nuruni. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana hakuna neno lililositirika, ila kusudi lije kudhihirika; wala hakuna lililofichwa, ila kusudi lije kutokea wazi. |
Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
Kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kuwekwa wazi.
Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.