Maana BWANA awaambia hivi watu wa Yuda na Yerusalemu Ulimeni udongo katika konde zenu, wala msipande mbegu kati ya miiba.
Marko 4:18 - Swahili Revised Union Version Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba; ni watu walisikiao lile neno, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wengine ni kama zile mbegu zilizoanguka penye miti ya miiba. Huo ni mfano wa wale wanaosikia hilo neno, Biblia Habari Njema - BHND Watu wengine ni kama zile mbegu zilizoanguka penye miti ya miiba. Huo ni mfano wa wale wanaosikia hilo neno, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wengine ni kama zile mbegu zilizoanguka penye miti ya miiba. Huo ni mfano wa wale wanaosikia hilo neno, Neno: Bibilia Takatifu Lakini wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye miiba, hulisikia lile neno; Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye miiba, hulisikia lile neno; BIBLIA KISWAHILI Na hawa ndio wale wapandwao penye miiba; ni watu walisikiao lile neno, |
Maana BWANA awaambia hivi watu wa Yuda na Yerusalemu Ulimeni udongo katika konde zenu, wala msipande mbegu kati ya miiba.
Naye aliyepandwa penye miiba, huyo ndiye alisikiaye lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai.
ila hawana mizizi ndani yao, bali hudumu muda mchache; kisha ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara hujikwaa.
na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai.
Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lolote.