Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Marko 16:10 - Swahili Revised Union Version Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wapokuwa wanaomboleza na kulia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maria Magdalene akaenda, akawajulisha wale waliokuwa pamoja na Yesu, na wakati huo walikuwa wanaomboleza na kulia. Biblia Habari Njema - BHND Maria Magdalene akaenda, akawajulisha wale waliokuwa pamoja na Yesu, na wakati huo walikuwa wanaomboleza na kulia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maria Magdalene akaenda, akawajulisha wale waliokuwa pamoja na Yesu, na wakati huo walikuwa wanaomboleza na kulia. Neno: Bibilia Takatifu Mariamu akaenda, naye akawaambia wale waliokuwa wamefuatana na Isa, waliokuwa wanaomboleza na kulia. Neno: Maandiko Matakatifu Maria akaenda, naye akawaambia wale waliokuwa wamefuatana na Isa, waliokuwa wanaomboleza na kulia. BIBLIA KISWAHILI Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao walikuwa wanaomboleza na kulia. |
Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.
Na mara jogoo akawika mara ya pili. Petro akalikumbuka lile neno aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu. Na alipolifikiri, akalia.
Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao.
Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo.