Marko 15:45 - Swahili Revised Union Version Hata alipokwisha kupata hakika kutoka kwa yule kamanda, alimpa Yusufu yule maiti. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu kuuchukua mwili wake. Biblia Habari Njema - BHND Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu kuuchukua mwili wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu kuuchukua mwili wake. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yusufu ruhusa ya kuuchukua huo mwili. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yusufu ruhusa ya kuuchukua huo mwili. BIBLIA KISWAHILI Hata alipokwisha kupata hakika kutoka kwa yule kamanda, alimpa Yusufu yule maiti. |
Basi yule kamanda, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
Lakini Pilato akastaajabu, kama amekwisha kufa. Akamwita yule kamanda, akamwuliza kwamba amekufa kitambo.
Naye akanunua sanda ya kitani, akamteremsha, akamfungia ile sanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani; akavingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi.
Hata baada ya hayo Yusufu wa Arimathaya, naye ni mwanafunzi wa Yesu, (lakini kwa siri, kwa hofu ya Wayahudi), alimwomba Pilato ruhusa ili auondoe mwili wake Yesu. Na Pilato akampa ruhusa. Basi akaenda, akauondoa mwili wake.