Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
Marko 14:39 - Swahili Revised Union Version Akaenda zake tena, akaomba, akisema neno lilo hilo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akaenda kusali tena akirudia maneno yaleyale. Biblia Habari Njema - BHND Akaenda kusali tena akirudia maneno yaleyale. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akaenda kusali tena akirudia maneno yaleyale. Neno: Bibilia Takatifu Akaenda tena kuomba, akisema maneno yale yale. Neno: Maandiko Matakatifu Akaenda tena kuomba, akisema maneno yale yale. BIBLIA KISWAHILI Akaenda zake tena, akaomba, akisema neno lilo hilo. |
Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
Akaja tena akawakuta wamelala, maana macho yao yamekuwa mazito, wala hawakujua la kumjibu.
Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;