Ukiwatesa watu hao katika neno lolote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,
Maombolezo 5:3 - Swahili Revised Union Version Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; Mama zetu wamekuwa kama wajane. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tumekuwa yatima, bila baba, mama zetu wameachwa kama wajane. Biblia Habari Njema - BHND Tumekuwa yatima, bila baba, mama zetu wameachwa kama wajane. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tumekuwa yatima, bila baba, mama zetu wameachwa kama wajane. Neno: Bibilia Takatifu Tumekuwa yatima wasio na baba, mama zetu wamekuwa kama wajane. Neno: Maandiko Matakatifu Tumekuwa yatima wasio na baba, mama zetu wamekuwa kama wajane. BIBLIA KISWAHILI Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; Mama zetu wamekuwa kama wajane. |
Ukiwatesa watu hao katika neno lolote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,
na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.
Wajane wao wameongezeka kwangu kuliko mchanga wa bahari; nimeleta mwenye kuteka wakati wa adhuhuri juu ya mama wa vijana; nimeleta uchungu na hofu kuu impate ghafla.
Kwa sababu hiyo, uwatoe watoto wao waone njaa, uwatoe nguvu za upanga ziwapate; wake zao wafiwe na watoto wao, na kufiwa na waume zao; wanaume wao wauawe, na vijana wao wapigwe kwa upanga vitani.
Ashuru hatatuokoa; hatutapanda farasi; wala hatutaiambia tena kazi ya mikono yetu, Ninyi ndinyi miungu yetu; maana kwako wewe wasio na baba hupata rehema.