Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 15:8 - Swahili Revised Union Version

8 Wajane wao wameongezeka kwangu kuliko mchanga wa bahari; nimeleta mwenye kuteka wakati wa adhuhuri juu ya mama wa vijana; nimeleta uchungu na hofu kuu impate ghafla.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Wajane wao wamekuwa wengi kuliko mchanga wa bahari. Kina mama wa watoto walio vijana nimewaletea mwangamizi mchana. Nimesababisha uchungu na vitisho viwapate kwa ghafla.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Wajane wao wamekuwa wengi kuliko mchanga wa bahari. Kina mama wa watoto walio vijana nimewaletea mwangamizi mchana. Nimesababisha uchungu na vitisho viwapate kwa ghafla.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Wajane wao wamekuwa wengi kuliko mchanga wa bahari. Kina mama wa watoto walio vijana nimewaletea mwangamizi mchana. Nimesababisha uchungu na vitisho viwapate kwa ghafla.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Nitawafanya wajane wao kuwa wengi kuliko mchanga wa bahari. Wakati wa adhuhuri nitamleta mwangamizi dhidi ya mama wa vijana wao wa kiume; kwa ghafula nitaleta juu yao maumivu makuu na hofu kuu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Nitawafanya wajane wao kuwa wengi kuliko mchanga wa bahari. Wakati wa adhuhuri nitamleta mharabu dhidi ya mama wa vijana wao waume; kwa ghafula nitaleta juu yao maumivu makuu na hofu kuu.

Tazama sura Nakili




Yeremia 15:8
15 Marejeleo ya Msalaba  

Watu wako wanaume wataanguka kwa upanga, na mashujaa wako vitani.


Na malango yake yatalia na kuomboleza, naye atakuwa ukiwa, atakaa chini.


Na siku hiyo wanawake saba watamshika mwanaume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.


Maana BWANA asema hivi, kuhusu habari za wana, na kuhusu habari za binti, wazaliwao mahali hapa, na kuhusu habari za mama zao waliowazaa, na kuhusu habari za baba zao waliowazaa, katika nchi hii;


Kwa sababu hiyo, uwatoe watoto wao waone njaa, uwatoe nguvu za upanga ziwapate; wake zao wafiwe na watoto wao, na kufiwa na waume zao; wanaume wao wauawe, na vijana wao wapigwe kwa upanga vitani.


Nami nitawatayarisha waangamizi juu yako, kila mtu na silaha zake; Nao watakata mierezi yako miteule, na kuitupa motoni.


Wapasheni mataifa habari; angalieni, hubirini juu ya Yerusalemu, ya kwamba walinzi wanatoka katika nchi ya mbali, wanatoa sauti yao juu ya miji ya Yuda.


Basi, kwa hiyo, simba atokaye mwituni atawaua, mbwamwitu wa jioni atawateka, chui ataivizia miji yao, kila mtu atokaye humo atararuliwa vipande vipande; kwa sababu makosa yao ni mengi, na kurudi nyuma kwao kumezidi.


Ee binti wa watu wangu, ujivike nguo ya magunia, na kugaagaa katika majivu; fanya maombolezo, kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, maombolezo ya uchungu mwingi; maana mwenye kuteka nyara atakuja juu yetu ghafla.


Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; Mama zetu wamekuwa kama wajane.


Fitina ya manabii wake imo ndani yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo; wamekula roho za watu; hutwaa kwa nguvu hazina na vitu vya thamani; wameongeza idadi ya wajane wake ndani yake.


Na wewe utajikwaa wakati wa mchana, na nabii naye atajikwaa pamoja nawe wakati wa usiku; nami nitamwangamiza mama yako.


kwa kuwa ndivyo itakavyowajia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo