Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 15:9 - Swahili Revised Union Version

9 Mwanamke aliyezaa watoto saba anazimia; ametoa roho; jua lake limekuchwa, ikiwa bado ni wakati wa mchana; ameaibika na kutwezwa; na mabaki yao nitawatoa kwa upanga mbele ya adui zao, asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Mama aliyesifika kuwa na watoto saba; sasa ghafla hana kitu. Ametoa pumzi yake ya mwisho, jua lake limetua kukiwa bado mchana; ameaibishwa na kufedheheshwa. Na wale waliobaki hai nitawaacha wauawe kwa upanga na maadui zao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Mama aliyesifika kuwa na watoto saba; sasa ghafla hana kitu. Ametoa pumzi yake ya mwisho, jua lake limetua kukiwa bado mchana; ameaibishwa na kufedheheshwa. Na wale waliobaki hai nitawaacha wauawe kwa upanga na maadui zao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Mama aliyesifika kuwa na watoto saba; sasa ghafla hana kitu. Ametoa pumzi yake ya mwisho, jua lake limetua kukiwa bado mchana; ameaibishwa na kufedheheshwa. Na wale waliobaki hai nitawaacha wauawe kwa upanga na maadui zao. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Mama mwenye watoto saba atazimia na kupumua pumzi yake ya mwisho. Jua lake litatua kukiwa bado mchana, atatahayarika na kufedheheka. Wale wote waliobaki nitawaua kwa upanga mbele ya adui zao,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Mama mwenye watoto saba atazimia na kupumua pumzi yake ya mwisho. Jua lake litatua kungali bado mchana, atatahayarika na kufedheheka. Wale wote waliobaki nitawaua kwa upanga mbele ya adui zao,” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 15:9
14 Marejeleo ya Msalaba  

lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kamili, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na uganga wako mwingi mno.


Nami nitalitangua shauri la Yuda na Yerusalemu mahali hapa; nami nitawaangusha kwa upanga mbele za adui zao, na kwa mkono wa watu watafutao roho zao; na mizoga yao nitawapa ndege wa angani na wanyama wakali wa nchi, iwe chakula chao.


Na baada ya hayo, asema BWANA, nitamtia Sedekia, mfalme wa Yuda, na watumishi wake, na watu wote waliosalia ndani ya mji huu, baada ya tauni ile, na upanga, na njaa, katika mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao; naye atawaua kwa ukali wa upanga; hatawaachilia, wala hatawahurumia, wala hatawarehemu.


Tazama, nawaangalia niwaletee mabaya, wala si mema; nao watu wote wa Yuda, walioko hapa katika nchi ya Misri, wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa, hadi wakomeshwe kabisa.


mama yenu atatahayarika sana; yeye aliyewazaa atafadhaika; tazama, atakuwa taifa lililo nyuma katika mataifa yote, atakuwa jangwa, nchi ya ukame, na nyika.


Takaseni vita juu yake; inukeni, na tupande juu wakati wa adhuhuri. Ole wetu, kwa kuwa mchana umeanza kupungua, vivuli vya jioni vinazidi kuwa virefu.


Je! Watu hawa wanikasirisha mimi? Asema BWANA; hawajikasirishi nafsi zao, na kuzitia haya nyuso zao wenyewe?


Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa!


Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu.


Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma yao.


Hivyo ndivyo ghadhabu yangu itakavyotimia, nami nitatosheleza hasira yangu juu yao, nami nitafarijika; nao watajua ya kuwa mimi, BWANA, nimenena kwa wivu wangu, nitakapokuwa nimeitimiza ghadhabu yangu juu yao.


Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula, Lakini waliokuwa na njaa sasa hawana njaa tena. Naam, huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba, lakini aliye na watoto wengi amehuzunika.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo