Maombolezo 5:2 - Swahili Revised Union Version Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni; Na nyumba zetu kuwa mali ya mataifa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nchi yetu imekabidhiwa wageni, nyumba zetu watu wengine. Biblia Habari Njema - BHND Nchi yetu imekabidhiwa wageni, nyumba zetu watu wengine. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nchi yetu imekabidhiwa wageni, nyumba zetu watu wengine. Neno: Bibilia Takatifu Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni, na nyumba zetu kwa wageni. Neno: Maandiko Matakatifu Urithi wetu umegeuziwa kwa wageni, na nyumba zetu kwa wageni. BIBLIA KISWAHILI Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni; Na nyumba zetu kuwa mali ya mataifa. |
Nchi yenu ni ukiwa; miji yenu imeteketezwa kwa moto; nchi yenu, wageni wameila mbele ya macho yenu; nayo ni ukiwa, kana kwamba imeangamizwa na wageni.
Ndipo wana-kondoo watakapojilisha kama walio katika malisho yao wenyewe, na mahali pao walionenepa, palipoachwa ukiwa, wageni watakula.
Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako.
Nawe, naam, wewe nafsi yako, utaachana na urithi wako niliokupa; nami nitakulazimisha kuwatumikia adui zako katika nchi usiyoijua; maana umewasha moto katika hasira yangu, utakaowaka milele.
Na nyumba zao zitakuwa mali za watu wengine, mashamba yao na wake zao pamoja; kwa kuwa nitaunyosha mkono wangu juu ya wenyeji wa nchi hii, asema BWANA.
Nami nitapatia katika mikono ya wageni pawe mateka yao, na katika mikono ya waovu wa duniani pawe mawindo yao, nao watapanajisi.
Kwa sababu hiyo nitawaleta watu wa mataifa walio wabaya kabisa, nao watazimiliki nyumba zao; tena nitakikomesha kiburi chao wenye nguvu; na mahali pao patakatifu patatiwa unajisi.
Kwa maana wao hupanda upepo, nao watavuna tufani; nafaka haina bua; machipuko yake hayatoi masuke; hata ikiwa yatoa, wageni watayameza.
Na huko utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao zitakuwa ukiwa; naam, watajenga nyumba, lakini hawatakaa ndani yake; nao watapanda mizabibu, lakini hawatakunywa divai yake.