Enyi binti za Israeli, mlilieni Huyo Sauli, ambaye aliwavika Mavazi mekundu kwa anasa, Akazipamba nguo zenu dhahabu.
Maombolezo 4:5 - Swahili Revised Union Version Wale waliokula vitu vya anasa Wameachwa peke yao njiani; Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekundu Wakumbatia jaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu waliojilisha vyakula vinono sasa wanakufa njaa barabarani. Waliolelewa na kuvikwa kifalme sasa wanafukua kwa mikono kwenye majaa. Biblia Habari Njema - BHND Watu waliojilisha vyakula vinono sasa wanakufa njaa barabarani. Waliolelewa na kuvikwa kifalme sasa wanafukua kwa mikono kwenye majaa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu waliojilisha vyakula vinono sasa wanakufa njaa barabarani. Waliolelewa na kuvikwa kifalme sasa wanafukua kwa mikono kwenye majaa. Neno: Bibilia Takatifu Wale waliokula vyakula vya kifahari ni maskini barabarani. Wale waliokuzwa wakivaa nguo za zambarau sasa wanalalia majivu. Neno: Maandiko Matakatifu Wale waliokula vyakula vya kifahari ni maskini barabarani. Wale waliokuzwa wakivaa nguo za zambarau sasa wanalalia majivu. BIBLIA KISWAHILI Wale waliokula vitu vya anasa Wameachwa peke yao njiani; Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekundu Wakumbatia jaa. |
Enyi binti za Israeli, mlilieni Huyo Sauli, ambaye aliwavika Mavazi mekundu kwa anasa, Akazipamba nguo zenu dhahabu.
Lakini yule kamanda akawaambia, Je! Bwana wangu amenituma kwa bwana wako, na kwako wewe, niseme maneno haya? Je! Hakunituma kwa watu hawa walio ukutani, ili wale mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao pamoja nanyi?
Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamanio yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge.
Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu.
Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Jueni, watu wenye mavazi ya utukufu, wanaokaa kwa raha, wamo katika majumba ya kifalme.