Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Maombolezo 4:10 - Swahili Revised Union Version

Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kina mama ambao huwa na huruma kuu waliwapika watoto wao wenyewe, wakawafanya kuwa chakula chao wakati watu wangu walipoangamizwa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kina mama ambao huwa na huruma kuu waliwapika watoto wao wenyewe, wakawafanya kuwa chakula chao wakati watu wangu walipoangamizwa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kina mama ambao huwa na huruma kuu waliwapika watoto wao wenyewe, wakawafanya kuwa chakula chao wakati watu wangu walipoangamizwa.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa mikono yao wenyewe wanawake wenye huruma wanapika watoto wao wenyewe, waliokuwa chakula chao watu wangu walipoangamizwa.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa mikono yao wenyewe wanawake wenye huruma wanapika watoto wao wenyewe, waliokuwa chakula chao watu wangu walipoangamizwa.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Maombolezo 4:10
12 Marejeleo ya Msalaba  

Siku ya tisa ya mwezi wa nne njaa ilikuwa nzito ndani ya mji, hata hapakuwa na chakula kwa watu wa nchi.

Ewe uliyejaa makelele, Mji wa ghasia, mji wenye furaha; Watu wako waliouawa hawakuuawa kwa upanga, Wala hawakufa vitani.

Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.

Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawatesa.

Macho yangu yamechoka kwa machozi, Mtima wangu umetaabika; Ini langu linamiminwa juu ya nchi Kwa uharibifu wa binti ya watu wangu; Kwa sababu watoto wachanga na wanyonyao, Huzimia katika mitaa ya mji.

Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?

Jicho langu lachuruzika mito ya machozi Kwa sababu ya kuharibiwa kwa binti zangu.

Hata mbwamwitu hutoa matiti, Huwanyonyesha watoto wao; Binti ya watu wangu amekuwa mkali, Mfano wa mbuni jangwani.

Kwa sababu hiyo baba za watu watawala wana wao kati yako, nao wana watawala baba zao; nami nitafanya hukumu ndani yako, na hao wote waliosalia kwako nitawatawanya kwa pepo zote.

Nanyi mtakula nyama ya miili ya watoto wenu wa kiume, na nyama ya miili ya binti zenu mtaila.