Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Maombolezo 4:3 - Swahili Revised Union Version

3 Hata mbwamwitu hutoa matiti, Huwanyonyesha watoto wao; Binti ya watu wangu amekuwa mkali, Mfano wa mbuni jangwani.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Hata mbwamwitu huwa na hisia za mama na kuwanyonyesha watoto wao; lakini watu wangu wamekuwa wakatili, hufanya kama mbuni nyikani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Hata mbwamwitu huwa na hisia za mama na kuwanyonyesha watoto wao; lakini watu wangu wamekuwa wakatili, hufanya kama mbuni nyikani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Hata mbwamwitu huwa na hisia za mama na kuwanyonyesha watoto wao; lakini watu wangu wamekuwa wakatili, hufanya kama mbuni nyikani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Hata mbweha hutoa matiti yao kunyonyesha watoto wao, lakini watu wangu wamekuwa wasio na huruma kama mbuni jangwani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Hata mbweha hutoa matiti yao kunyonyesha watoto wao, lakini watu wangu wamekuwa wasio na huruma kama mbuni jangwani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Hata mbwamwitu hutoa matiti, Huwanyonyesha watoto wao; Binti ya watu wangu amekuwa mkali, Mfano wa mbuni jangwani.

Tazama sura Nakili

Maombolezo 4:3
14 Marejeleo ya Msalaba  

Nilipoamka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe. Amekufa. Na asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa.

Na mbwamwitu watalia ndani ya ngome zake; na mbweha ndani ya majumba ya anasa; na wakati wake u karibu kufika, na siku zake hazitaongezeka.

Miiba itamea majumbani mwake, upupu na mbigili ndani ya maboma yake; nayo itakuwa kao la mbweha, na ua la mbuni.

Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.

Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawatesa.

Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?

Mikono ya wanawake wenye huruma Imewatokosa watoto wao wenyewe; Walikuwa ndio chakula chao Katika uharibifu wa binti ya watu wangu.

Kwa sababu hiyo baba za watu watawala wana wao kati yako, nao wana watawala baba zao; nami nitafanya hukumu ndani yako, na hao wote waliosalia kwako nitawatawanya kwa pepo zote.

Nanyi mtakula nyama ya miili ya watoto wenu wa kiume, na nyama ya miili ya binti zenu mtaila.

wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo