Maombolezo 3:7 - Swahili Revised Union Version Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka; Amenifunga kwa mnyororo mzito. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amenizungushia ukuta nisitoroke, amenifunga kwa minyororo mizito. Biblia Habari Njema - BHND Amenizungushia ukuta nisitoroke, amenifunga kwa minyororo mizito. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amenizungushia ukuta nisitoroke, amenifunga kwa minyororo mizito. Neno: Bibilia Takatifu Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka, amenifunga kwa minyororo mizito. Neno: Maandiko Matakatifu Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka, amenifunga kwa minyororo mizito. BIBLIA KISWAHILI Amenizinga pande zote hata siwezi kutoka; Amenifunga kwa mnyororo mzito. |
Jicho langu limefifia kwa ajili ya mateso BWANA, ninakuita kila siku; Ninakunyoshea Wewe mikono yangu.
Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika ukumbi wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo.
Na sasa, tazama, nakufungulia leo minyororo hii iliyo mikononi mwako. Kama ukiona ni vema kwenda Babeli pamoja nami, haya! Njoo, nami nitakutunza sana; lakini kama ukiona ni vibaya kwenda Babeli pamoja nami, basi, acha; tazama, nchi yote iko mbele yako; palipo pema machoni pako na pa kukufaa, nenda huko.
Kongwa la makosa yangu limefungwa na mkono wake; Hayo yameshikamana; Yamepanda juu shingoni mwangu; Amezikomesha nguvu zangu;
Naye ameyathibitisha maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuzi wetu waliotuamua, kwa kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu.
Basi kwa ajili ya hayo, angalia, nitaiziba njia yako kwa miiba, nami nitafanya kitalu juu yake, asipate kuyaona mapito yake.