Maombolezo 3:62 - Swahili Revised Union Version Midomo yao walioinuka juu yangu Na maazimio yao juu yangu mchana kutwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maneno na mawazo ya maadui zangu siku nzima ni juu ya kuniangamiza mimi. Biblia Habari Njema - BHND Maneno na mawazo ya maadui zangu siku nzima ni juu ya kuniangamiza mimi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maneno na mawazo ya maadui zangu siku nzima ni juu ya kuniangamiza mimi. Neno: Bibilia Takatifu kile adui zangu wanachonong’ona na kunung’unikia dhidi yangu mchana kutwa. Neno: Maandiko Matakatifu kile adui zangu wanachonong’ona na kunung’unikia dhidi yangu mchana kutwa. BIBLIA KISWAHILI Midomo yao walioinuka juu yangu Na maazimio yao juu yangu mchana kutwa. |
Kwa dhambi ya kinywa chao, Na kwa neno la midomo yao, Wanaswe kwa kiburi chao, Kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao.
Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.
basi tabiri useme, Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu, naam, kwa sababu wamewafanya ninyi kuwa ukiwa, na kuwameza pande zote, mpate kuwa milki kwa mabaki ya mataifa, nanyi mmesemwa kwa midomo yao waongeao, na kwa masingizio ya watu;