Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.
Maombolezo 3:59 - Swahili Revised Union Version Umekuona kudhulumiwa kwangu, Ee BWANA; Unihukumie neno langu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Umeuona uovu niliotendewa ee Mwenyezi-Mungu, uniamulie kwa wema kisa changu. Biblia Habari Njema - BHND Umeuona uovu niliotendewa ee Mwenyezi-Mungu, uniamulie kwa wema kisa changu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Umeuona uovu niliotendewa ee Mwenyezi-Mungu, uniamulie kwa wema kisa changu. Neno: Bibilia Takatifu Umeona, Ee Mwenyezi Mungu, ubaya niliotendewa. Tetea shauri langu! Neno: Maandiko Matakatifu Umeona, Ee bwana, ubaya niliotendewa. Tetea shauri langu! BIBLIA KISWAHILI Umekuona kudhulumiwa kwangu, Ee BWANA; Unihukumie neno langu. |
Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.
Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Abrahamu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu.
Umeona, maana unaangalia matatizo na dhiki, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima.
Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.
Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu Kwa ajili ya madai yangu, Mungu wangu na Bwana wangu.
Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki, Uniokoe kutoka kwa mtu wa hila asiye haki.
Ole wangu, mama yangu, kwa kuwa umenizaa mtu wa kuteta, na mtu wa kushindana na dunia yote! Mimi sikukopesha kwa riba, wala watu hawakunikopesha kwa riba; lakini kila mmoja wao hunilaani.
Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.