Maombolezo 3:43 - Swahili Revised Union Version Umetufunika kwa hasira na kutufuatia; Umeua, wala hukuona huruma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Umejizungushia hasira yako ukatufuatia, ukatuua bila huruma. Biblia Habari Njema - BHND “Umejizungushia hasira yako ukatufuatia, ukatuua bila huruma. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Umejizungushia hasira yako ukatufuatia, ukatuua bila huruma. Neno: Bibilia Takatifu “Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia; umetuchinja bila huruma. Neno: Maandiko Matakatifu “Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia; umetuchinja bila huruma. BIBLIA KISWAHILI Umetufunika kwa hasira na kutufuatia; Umeua, wala hukuona huruma. |
BWANA ameyatenda aliyoyakusudia; amelitimiza neno lake, Aliloliamuru siku za kale; Ameangusha hata chini, Wala hakuona huruma; Naye amemfurahisha adui juu yako, Ameitukuza pembe ya watesi wako.
Kijana na mzee hulala chini Katika njia kuu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wameanguka kwa upanga; Umewaua katika siku ya hasira yako; Umeua, wala hukuona huruma.
Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, BWANA, napiga.
Kwa sababu hiyo mimi nami nitatenda kwa ghadhabu; jicho langu halitaachilia, wala sitawaonea huruma, na wajapolia masikioni mwangu kwa sauti kuu, sitawasikiliza.
Nami, jicho langu halitaachilia, wala sitakuwa na huruma; lakini nitaleta njia yao juu ya vichwa vyao.