Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Maombolezo 2:17 - Swahili Revised Union Version

17 BWANA ameyatenda aliyoyakusudia; amelitimiza neno lake, Aliloliamuru siku za kale; Ameangusha hata chini, Wala hakuona huruma; Naye amemfurahisha adui juu yako, Ameitukuza pembe ya watesi wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Mwenyezi-Mungu amefanya yale aliyokusudia, ametekeleza yale aliyotishia; kama alivyopanga tangu kale ameangamiza bila huruma yoyote; amewafanya maadui wafurahie adhabu yako, amewakuza mashujaa wa maadui zako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Mwenyezi-Mungu amefanya yale aliyokusudia, ametekeleza yale aliyotishia; kama alivyopanga tangu kale ameangamiza bila huruma yoyote; amewafanya maadui wafurahie adhabu yako, amewakuza mashujaa wa maadui zako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Mwenyezi-Mungu amefanya yale aliyokusudia, ametekeleza yale aliyotishia; kama alivyopanga tangu kale ameangamiza bila huruma yoyote; amewafanya maadui wafurahie adhabu yako, amewakuza mashujaa wa maadui zako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Mwenyezi Mungu amefanya lile alilolipanga; ametimiza neno lake aliloliamuru siku za kale. Amekuangusha bila huruma, amewaacha adui wakusimange, ametukuza pembe ya adui yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 bwana amefanya lile alilolipanga; ametimiza neno lake aliloliamuru siku za kale. Amekuangusha bila huruma, amewaacha adui wakusimange, ametukuza pembe ya adui yako.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

17 BWANA ameyatenda aliyoyakusudia; amelitimiza neno lake, Aliloliamuru siku za kale; Ameangusha hata chini, Wala hakuona huruma; Naye amemfurahisha adui juu yako, Ameitukuza pembe ya watesi wako.

Tazama sura Nakili




Maombolezo 2:17
28 Marejeleo ya Msalaba  

basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote.


Unihukumu kwa haki yako, Ee BWANA, Mungu wangu, Na usiwaache wanisimange.


Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu.


Maana nilisema, Wasije wakanifurahia; Wale wanaojitukuza juu yangu Mguu wangu unapoteleza.


Umeutukuza mkono wa kulia wa watesi wake; Umewafurahisha wote wanaomchukia.


Pia umeurudisha nyuma ukali wa upanga wake; Wala hukumsimamisha vitani.


Msifurahi, Enyi Wafilisti wote, Kwa sababu fimbo ile iliyokupiga imevunjika; Maana katika shina la nyoka atatoka fira, Na uzao wake ni joka la moto arukaye Sef 2:4-7; Zek 9:5-7


Haya! Basi, ukawaambie watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu, ukisema, BWANA asema hivi, Tazama, ninafinyanga mabaya juu yenu, na kuwaza mawazo juu yenu; rudini sasa, kila mmoja na aiache njia yake mbaya; zitengenezeni njia zenu, na matendo yenu.


Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza, na mbingu zitakuwa nyeusi; kwa sababu mimi nimeyanena haya, na kuyakusudia, wala sikujuta wala mimi sitarudi nyuma niyaache.


naye BWANA ameyaleta, na kufanya kama alivyosema; kwa sababu mmemwasi BWANA, wala hamkuitii sauti yake; ndiyo maana neno hili limewajia ninyi.


Watesi wake wamekuwa kichwa, Adui zake hufanikiwa; Kwa kuwa BWANA amemtesa Kwa sababu ya wingi wa makosa yake; Watoto wake wadogo wamechukuliwa mateka Mbele yake huyo mtesi.


BWANA amekusudia kuuharibu Ukuta wa binti Sayuni; Ameinyosha hiyo kamba, Hakuuzuia mkono wake usiangamize; Bali amefanya boma na ukuta kuomboleza; Zote pamoja hudhoofika.


Umetufunika kwa hasira na kutufuatia; Umeua, wala hukuona huruma.


BWANA ameitimiza ghadhabu yake, Ameimimina hasira yake kali; Naye amewasha moto katika Sayuni Ulioiteketeza misingi yake.


Kwa sababu hiyo, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa kuwa umepatia unajisi patakatifu pangu, kwa matendo yako yote niyachukiayo, na kwa machukizo yako yote, kwa sababu hiyo mimi nami nitakupunguza; wala jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma.


Kwa sababu hiyo mimi nami nitatenda kwa ghadhabu; jicho langu halitaachilia, wala sitawaonea huruma, na wajapolia masikioni mwangu kwa sauti kuu, sitawasikiliza.


Nami, jicho langu halitaachilia, wala sitakuwa na huruma; lakini nitaleta njia yao juu ya vichwa vyao.


Naye ameyathibitisha maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuzi wetu waliotuamua, kwa kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu.


Basi BWANA asema hivi, Angalia, nakusudia jambo baya juu ya jamaa hii, ambalo hamtazitoa shingo zenu, wala hamtakwenda kwa kiburi; kwa maana ni wakati mbaya.


Nitavikomesha kabisa vitu vyote, visionekane juu ya uso wa nchi, asema BWANA.


Lakini maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je, Hazikuwapata baba zenu? Nao wakatubu na kusema, BWANA wa majeshi ametutenda kulingana na njia zetu, na matendo yetu, kama alivyokusudia kutenda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo