Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Maombolezo 3:40 - Swahili Revised Union Version

Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu, Na kumrudia BWANA tena.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Na tupime na kuchunguza mwenendo wetu, tupate kumrudia Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Na tupime na kuchunguza mwenendo wetu, tupate kumrudia Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Na tupime na kuchunguza mwenendo wetu, tupate kumrudia Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie Mwenyezi Mungu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie bwana Mwenyezi Mungu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Na tuchunguze njia zetu na kuzijaribu, Na kumrudia BWANA tena.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Maombolezo 3:40
22 Marejeleo ya Msalaba  

Matarishi, kwa amri ya mfalme na maofisa wake wakapeleka nyaraka katika Israeli na Yuda yote, kusema, Enyi wana wa Israeli, mrudieni BWANA, Mungu wa Abrahamu, na Isaka, na Israeli, apate kuwarudia ninyi mlionusurika na kuokoka toka mikononi mwa Wafalme wa Ashuru.


Kwa kuwa mkimrudia BWANA, ndugu zenu na watoto wenu watahurumiwa machoni pa hao waliowachukua mateka, nao watairudia nchi hii; kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye mwenye neema, na mwenye rehema, wala hatawageuzia mbali uso wake, mkimrudia.


Ninapozitafakari njia zako, Naielekeza miguu yangu kwa shuhuda zako.


Muwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.


Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.


Kwa sababu atafakari, na kughairi, na kuyaacha makosa yake yote aliyoyatenda, hakika ataishi, hatakufa.


Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.


Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.


Njooni, tumrudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga majeraha yetu.


bali kwanza niliwahubiria wale wa Dameski na Yerusalemu, na katika nchi yote ya Yudea, na watu wa Mataifa, kwamba watubu na kumwelekea Mungu, wakiyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao.


Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.


Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa.


Jichunguzeni wenyewe muone kama mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa iwe mmekataliwa.


Na wakati uwapo katika mashaka, ukiisha kupatwa na mambo haya yote, siku za mwisho, utamrudia BWANA, Mungu wako, na kuisikiza sauti yake;