Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa, akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe, akamzalia mtoto wa kiume. Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza BWANA.
Maombolezo 3:36 - Swahili Revised Union Version Na kumnyima mtu haki yake, Hayo Bwana hayaridhii kabisa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kesi ya mtu inapopotoshwa mahakamani, je, Mwenyezi-Mungu haoni hayo? Biblia Habari Njema - BHND kesi ya mtu inapopotoshwa mahakamani, je, Mwenyezi-Mungu haoni hayo? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kesi ya mtu inapopotoshwa mahakamani, je, Mwenyezi-Mungu haoni hayo? Neno: Bibilia Takatifu kumnyima mtu haki: Je, Bwana asione mambo kama haya? Neno: Maandiko Matakatifu kumnyima mtu haki: Je, Bwana asione mambo kama haya? BIBLIA KISWAHILI Na kumnyima mtu haki yake, Hayo Bwana hayaridhii kabisa. |
Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa, akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe, akamzalia mtoto wa kiume. Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza BWANA.
Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?
Naam, kweli imepunguka kabisa, na yeye auachaye uovu ajifanya kuwa mateka; naye BWANA akaona hayo, akachukizwa kwa kuwa hapana hukumu ya haki.
BWANA asema hivi, Fanyeni hukumu na haki, mkamtoe yeye aliyetekwa katika mikono ya mdhalimu; wala msiwatende mabaya mgeni, wala yatima, wala mjane, wala kuwadhulumu, wala msimwage damu ya mtu asiye na hatia katika mahali hapa.
Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;
Pakiwa na mashindano kati ya watu, wakaenda maamuzini, na hao waamuzi wakawaamua; na wampe haki mwenye haki, na wamhukumie makosa yule mwovu;