Wamenifumbulia vinywa vyao; Wamenipiga shavuni kwa kunitukana; Hukutana pamoja juu yangu.
Maombolezo 3:30 - Swahili Revised Union Version Na amwelekezee yule ampigaye shavu lake; Ashibishwe mashutumu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yampasa kumgeuzia shavu mwenye kumpiga, na kuwa tayari kupokea matusi yake. Biblia Habari Njema - BHND Yampasa kumgeuzia shavu mwenye kumpiga, na kuwa tayari kupokea matusi yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yampasa kumgeuzia shavu mwenye kumpiga, na kuwa tayari kupokea matusi yake. Neno: Bibilia Takatifu Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye, na ajazwe na aibu. Neno: Maandiko Matakatifu Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye, na ajazwe na aibu. BIBLIA KISWAHILI Na amwelekezee yule ampigaye shavu lake; Ashibishwe mashutumu. |
Wamenifumbulia vinywa vyao; Wamenipiga shavuni kwa kunitukana; Hukutana pamoja juu yangu.
Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
Niliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang'oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.
Sasa utajikusanya vikosi vikosi, Ee binti wa vikosi; yeye amemhusuru; watampiga mwamuzi wa Israeli shavuni mwake kwa fimbo.
Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili.
Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
Maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani, akiwameza, akiwateka nyara, akijikuza, akiwapiga usoni.