Maombolezo 3:23 - Swahili Revised Union Version Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila kunapokucha ni mpya kabisa, uaminifu wake ni mkuu mno. Biblia Habari Njema - BHND Kila kunapokucha ni mpya kabisa, uaminifu wake ni mkuu mno. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila kunapokucha ni mpya kabisa, uaminifu wake ni mkuu mno. Neno: Bibilia Takatifu Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu. Neno: Maandiko Matakatifu Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu. BIBLIA KISWAHILI Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. |
Maana ghadhabu zake ni za muda mfupi tu; Radhi yake ni ya milele. Kilio huweza kuwapo usiku, Lakini furaha huja asubuhi.
Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee BWANA, unawalinda wanadamu na wanyama.
BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;
Ee BWANA, uturehemu; tumekungoja wewe; uwe wewe mkono wetu kila asububi, na wokovu wetu pia wakati wa taabu.
BWANA kati yake ni mwenye haki; hatatenda uovu; kila asubuhi hudhihirisha hukumu yake, wala hakomi; bali mtu asiye haki hajui kuona haya.
katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele;
ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;