Maombolezo 3:2 - Swahili Revised Union Version Ameniongoza na kunipeleka katika giza Wala si katika nuru. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amenichukua akanipeleka mpaka gizani kusiko na mwanga. Biblia Habari Njema - BHND Amenichukua akanipeleka mpaka gizani kusiko na mwanga. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amenichukua akanipeleka mpaka gizani kusiko na mwanga. Neno: Bibilia Takatifu Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee gizani wala si katika nuru; Neno: Maandiko Matakatifu Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee gizani wala si katika nuru; BIBLIA KISWAHILI Ameniongoza na kunipeleka katika giza Wala si katika nuru. |
Kwa sababu hiyo hukumu ya haki iko mbali nasi, wala haki haitufikii; twatazamia nuru, na kumbe! Latokea giza; twatazamia mwanga, lakini twaenda katika giza kuu.
Mtukuzeni BWANA, Mungu wenu, kabla hajaleta giza, na kabla miguu yenu haijakwaa juu ya milima yenye giza; na wakati mnapoitazamia nuru, kabla hajaigeuza kuwa kivuli cha mauti, na giza nene.
Niliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; niliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru.
Jinsi Bwana alivyomfunika binti Sayuni Kwa wingu katika hasira yake! Ameutupa toka mbinguni hata nchi Huo uzuri wa Israeli; Wala hakukikumbuka kiti cha miguu yake Katika siku ya hasira yake.
utakwenda kwa kupapasapapasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele.
Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.