Maombolezo 3:10 - Swahili Revised Union Version Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye, Kama simba aliye mafichoni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye ni kama dubu anayenivizia; ni kama simba aliyejificha. Biblia Habari Njema - BHND Yeye ni kama dubu anayenivizia; ni kama simba aliyejificha. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye ni kama dubu anayenivizia; ni kama simba aliyejificha. Neno: Bibilia Takatifu Kama dubu aviziaye, kama simba mafichoni, Neno: Maandiko Matakatifu Kama dubu aviziaye, kama simba mafichoni, BIBLIA KISWAHILI Alivyo kwangu ni kama dubu aoteaye, Kama simba aliye mafichoni. |
Huotea faraghani kama simba pangoni, Huotea amkamate mtu mnyonge. Naam, humkamata mtu mnyonge, Na kumkokota akiwa wavuni mwake.
Nilijituliza hata asubuhi; kama simba, anaivunja mifupa yangu yote; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
Maana mimi nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama mwanasimba kwa nyumba ya Yuda; mimi, naam, mimi nitararua, kisha nitakwenda zangu; nitachukua mbali, wala hapatakuwa na mtu wa kuokoa.
Njooni, tumrudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga majeraha yetu.